Pages

Friday, August 21, 2015

TWIGA STARS KUCHEZA JUMAPILI NA TFF YATUPA SALAMU ZA RAMBIRAMBI PWANI NA YANGA



TIMU ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania ‘Twiga Stars kesho watajipima nguvu na akina dada wenzao wa Kenya ‘Harambee Starlets’ katika Uwanja wa Amani kisiwani Zanzibar,
Akizungumza na wandishi wa habari leo, Afisa habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), alisema Harambee Starlets imewasili Zanzibar ikiwa na kikosi cha wachezaji 17 pamoja na viongozi 9 tayari kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya Twiga Stars siku ya jumapili.
“Twiga stars ambayo inajiandaa na fainali za Afrika zitakazofanyika Congo Brazaville itacheza mchezo wa kirafiki jumapili na timu ya wanawake ya Kenya”, alisema Kizuguto.
Mchezo huo wa kirafiki unatarajiwa kuanza majira ya saa 10 kamili jioni ambapo viingilio vitakuwa ni 2000 kwa jukwaa kuu, na 1000 kwa mzunguko.
Twiga Stars ambayo ilikata tiketi ya kucheza fainali za Afrika zinazotarajiwa kuanza Septemba 4-9 mwaka huu baada ya kuitoa Zambia ipo kundi moja na wenyeji Congo Brazavile, Nigeria na Ghana.
Wakati huohuo TFF imetuma salamu za rambi rambi kwa chama cha mpira wa miguu mkoa wa Pwani (COREFA) kufuatia kifo cha mwamuzi mstaafu wa mpira miguu Rajabu Zarara kilichotokea juzi jijini Dar es salam.
Marehemu Zarara licha ya kuwa mwamuzi alikuwa Mjumbe wa Kamati ya Waamuzi mkoa wa Pwani, amezikwa hapa jijini Dar es salaam.
 Pia TFF imetuma salamu za rambi rambi kwa Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, kufuatia kifo cha mwanachama wake Athuman Makaranga kilichotokea leo asubuhi jijni Dar es salaam.
TFF kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu nchini inawapa pole wafiwa, ndugu, jamaa na marafiki wote kufuatia misiba hiyo na kusema iko pamoja nao katika kipindi hiki cha maombolezo.

No comments:

Post a Comment