Kipa wa Kimataifa wa Argentina Sergio Romero ataendelea kuwa Golini kama alivyofanya Jumamosi iliyopita huko Old Trafford Man United ilipoifunga Tottenham 1-0 katika Mechi yao ya kwanza ya Ligi Kuu England kwa Msimu mpya wa 2015/16.
Hivi sasa Kipa David De Gea yupo kwenye sakata kubwa la kutaka kuhamia Real Madrid huku Man United ikitia ngumu na kutaka kitita kikubwa.
Van Gaal ameeleza kuwa Msimu uliopita wao walikuwa bora Nyumbani Old Trafford na rekodi hiyo iliwafanya wawe wa 3 katika Timu zilizofanya vizuri Nyumbani kwenye Ligi.
Meneja huyo pia alihojiwa kuhusu matamshi ya Straika wa zamani wa Barcelona Hristo Stoichkov ambae amemtaka Pedro kutohamia Man United kwa sababu yake yeye Van Gaal.
Stoichkov, aliecheza chini ya Van Gaal katika Miaka ya 1990 huko Barca, amedai Van Gaal huzibomoa Klabu kwa sababu ya uduni wake.
Huku Manchester City na Chelsea wakipambana huko Etihad hapo Jumapili, Waandishi walidokeza kuwa ushindi kwa Man United Ijumaa huko Villa Park utawafanya wachepuke haraka mbele ya Vigogo hao lakini Van Gaal alisema: “Ushindi utatupa mwanzo mzuri kupita Msimu uliopita. Lakini ni mapema na Msimu ni mrefu.”
Kuhusu Javier Hernandez ‘Chicharito’, Van Gaal alieleza: “Straika ni Rooney na Chicharito ni Straika wa Pili na yeye anajua hilo.”
No comments:
Post a Comment