Pages

Thursday, August 20, 2015

PEDRO AENDA CHELSEA

Fowadi wa Barcelona Pedro sasa atahamia Chelsea baada ya Klabu hiyo kukubali kulipa Pauni Milioni 22 kwa mkupuo kitu ambacho Manchester United waligomea kulipa.
Kwa muda mrefu iliaminika kuwa Pedro atatua Old Trafford huku kukiripotiwa kuwa tayari ameshaafikiana maslahi yake binafsi lakini kusita kwa Man United kulipa kwa mkupuo mmoja Dau ambalo Barca walikuwa wakitaka kumetoa mwanya kwa Chelsea kutumbukia na kukubali kulipa Dau hilo lote na kumnasa Staa huyo.

Man United walikuwa tayari kulipa Dau la Pauni Milioni 17.7 mbele na kisha kulipa pole pole Pauni Milioni 3.6 zikiwa nyongeza ambazo zitaendana na mafanikio atakayopata Mchezaji huyo akiwa na Man United.
Kitu hicho Barca waligomea na kutaka Fedha zote kwa mkupuo na hapo ndipo Chelsea wakawapiku Man United.
Inatarajiwa wakati wowote kuanzia sasa Pedro, mwenye Miaka 28, atapimwa Afya yake huko Stamford Bridge na kisha kusaini Mkataba.

No comments:

Post a Comment