Pages

Friday, August 21, 2015

MKWASA AITA 22 SAFARI YA UTURUKI



WACHEZAJI 22  wa timu ya Taifa ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) wanarajiwa kuondoka nchini kesho usiku kuelekea nchini Uturuki kwa kambi ya wiki moja kujiandaa na mchezo dhidi ya Nigeria utakaochezwa Septemba 05, 2015.
Akizungumza na wandishi wa habari leo, Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Baraka Kizuguto, alisema kuwa kocha mkuu wa Taifa Stars, Charles Mkwasa ametoa orodha ya wachezaji 22 watakaosafiri usiku wa jumapili.
“Orodha ya wachezaji 22 imetoka katika kikosi kilichotangazwa wiki mbili zilizopita na Mkwasa ambapo walipata nafasi ya kufanya mazoezi kwa takribani wiki moja katika uwanja wa Karume”, alisema Kizuguto.
Kizuguto alisema wachezaji wote waliochaguliwa kujiunga na timu ya Taifa wanapaswa kuripoti kambini Tansoma Hotel jumapili saa 5 asubuhi kwa maandalizi ya mwisho ya safari hiyo.
Wachezaji waliochaguliwa ni All Mustafa Aishi Manula, Said Mohamed, walinzi Shomari Kapombe, Abdi Banda, Mohamed Hussein, Hassan Isihaka, Juma Abdul, Haji Mngwali, Kelvin Yondani, Nadir Haroub.
Wengine ni Mudathir Yahya, Himid Mao, Frank Domayo, Salum Telela, Deus Kaseke, Said Ndemla, John Bocco, Farid Musa, , Rashid Mandawa, Saimon Msuva, na Ibrahim Ajib.
Taifa Stars kwa usafiri wa shirika la ndege la Uturuki (Turkish Airlines), na itafika jijini Istambul jumatatu asubuhi, ambapo itaelekea katika mji wa Kocael   kuweka kambi ya wiki moja katika hoteli ya Green Park Kartepe.

No comments:

Post a Comment