MSHAMBULIAJI
mkongwe wa Simba, Musa Hassan Mgosi ameteuliwa kuwa nahodha mpya wa timu hiyo
Mgosi amepewa ubosi huo na Kocha Mkuu wa
Simba, Muingereza, Dylan Kerr baada ya kuridhishwa na nidhamu pamoja na kiwango
cha Mgosi.
Awali
manahodha wa Simba walikuwa Hassan Isihaka na Jonas Mkude lakini kocha lakini
kocha ameangalia mtu mzoefu zaidi na anayehamasisha wenzake.
Akizungumza
jijini, Kocha msaidizi wa Simba SC, Seleman Matola amethibitisha uteuzi
huo na Mgosi ameteuliwa kuwa nahodha kutokana na uzoefu mkubwa.
“Kocha
ameangalia uzoefu, nahodha anatakiwa mtu kama Mgosi, anaweza kuongea na
wachezaji, anahamasisha timu, ndio maana ameteuliwa”.
Pia Matola
alisema timu inaweza kuwa na manahodha wanne, lakini Isihaka na Mkude wataendelea
kujifunza kwa Mgosi, pindi atakapoondoka wataweza kurithi nafasi yake.
No comments:
Post a Comment