JOSE MOURINHO AMKATAA DOKTA WA CHELSEA EVA CARNEIRO.
BAADA
ya kumlaumu sana Dokta wa Timu ya Chelsea, Eva Carneiro, mara baada ya
Mechi yao ya kwanza ya Ligi Kuu England Jumamosi iliyopita Uwanjani
Stamford Bridge waliyotoka 2-2 na Swansea City, Meneja Jose Mourinho
sasa ameamua Dokta huyo hatakaa tena na Benchi la Timu hiyo.
Inaaminika
Mwanamama Eva Carneiro atabakia Daktari wa Timu ya Kwanza ya Chelsea
lakini hataandamana na Timu kwenye Mechi wala kuhudhuria Mazoezi na
hivyo Jumapili ijayo hatatarajiwa kuwepo kwenye Benchi la Chelsea
wakicheza huko Etihad na Manchester City kama ilivyo kawaida yake.
Jumamosi
iliyopita, Uwanjani Stamford Bridge, katika Dakika za Majeruhi huku
Gemu na Swansea ikiwa 2-2 na Chelsea kuwa Mtu 10 baada ya Kipa wao
Thibaut Courtois kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu, Fowadi wa Chelsea Eden
Hazard alianguka chini kwa maumivu na Refa kuashiria Benchi la Chelsea
na ndipo Dokta Eva Carneiro akachomoka mbio kuingia Uwanjani kama
kawaida yake kwenda kutoa huduma.
Kitendo hicho kilimkera mno Mourinho na waziwazi alinaswa akimbatukia Dokta Eva Carneiro ambae nae alijibu mapigo.
Ghadhabu
za Mourinho zilitokana na Chelsea kubaki na wachezaji tisauwanjani kwa dakika
kadhaa kwani kisheria mchezaji akiumia ulazimika madaktari kuingia
kumtibu basi anapaswa kutoka nje ya uwanjani na mchezo kuendelea na baadae refa
kumruhusu arudi tena uwanjani.
Mourinho alidai Eva Carneiro hajui kusoma Mchezo.
Lakini,
katika kile kinachodaiwa kumkandya Mourinho hadharani, Dokta Eva
Carneiro aliposti kwenye kurasa yake ya facebook maneno haya: “Napenda
kuwashukuru Watu wote kwa sapoti yao. Natoa shukrani kubwa.”
Dokta
Eva Carneiro, ambae alizaliwa Septemba 15 Mwaka 1973 huko Gibraltar na
ambae Baba yake ni Mhispania na Mama Mwingereza, aliteuliwa kuwa Dokta
wa Timu ya Kwanza ya Chelsea Mwaka 2011 na aliekuwa Meneja wa wakati huo
Andre Villas-Boas.![](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_stVodSjgMcZMxkyiQzGnLZ0cCAYjC6k21stASgy8QJPxHxNlR-SuOzN5HvzK1vy7vk4iT9N53V9il-fY-S1PMwkhdqnEpbccvpDOnFMsRlVFo0VQmSVJ2kiWYUsAu5hbqpZ5lA3d0C8U2XpwtIFJGm4b5TRdyXKjxSj-x03ZTW4rNtzijIgDgQMStFrV-DjiOaaiXBDuo8kUFH9qw3AbJVU3VZenOJL-PehzpdvXwwLo2K8BUpRMuEz0afzEIYYr6s=s0-d)
No comments:
Post a Comment