Nyota
mpya wa Manchester United, Memphis Depay unaweza kusema amefanya
maamuzi magumu ya kuvaa viatu vizito. Kuelekea msimu ujao wa ligi kuu
England unaoanza Jumamosi hii, Depay ameomba kupewa jezi ya heshima Old
Trafford, namba 7. Mshambuliaji huyo kinda amejitosa kuchukua jezi hiyo
ya maana ambayo iliwahi kuvaliwa na masupastaa wa maana waliowahi
kucheza Manchester United wakiwemo George Best, Bryan Robson, Eric
Cantona, David Beckham na Cristiano Ronaldo na nyota wa sasa
anayeondoka, Angel di Maria. Inafahamika kwamba kocha wa United, Louis
van Gaal bado hajatoa namba katika kikosi chake. Namba 9 pia iko wazi,
lakini Van Gaal amevutiwa na maombi ya Depay kwani inaonesha jinsi gani
Mholanzi huyo anajiamini.Angel Di Maria aliyetimkia Klabu ya Matajiri PSG.
No comments:
Post a Comment