Pages

Wednesday, August 19, 2015

BFT YAMPONGEZA RAIS WAO KUTEULIWA KUGOMBEA UDIWANI KAWE CCM



SHIRIKISHO la Ngumi Tanzania (BFT) limempongeza Rais  wa Shirikisho hilo Robert Muta Rwakatale kwa kuchaguliwa kugombea udiwani  kupitia CCM.

Akizungumza na wandishi wa habari, Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga alisema kikao cha utendaji ya chama hicho kilichofanyika juzi kilimpongeza Rwakata

Katika  kikao cha  kamati ya  utendaji  cha  (BFT)  kilichofanyika katika Ofisi  za  BFT kiliomba kumpongeza Rwakatale kwa nafasi hiyo aliyoipata kupitia CCM  kata ya Kawe.

“BFT ina  imani kubwa na uongozi wake kwa kuwa amekuwa  imara kuhakikisha BFT inasonga mbele ingawa kuna changamoto mbalimbali za  kuongoza  vyama vya michezo hivyo BFT   inaamini kuwa  endapo atachaguliwa kuwa diwani atashirikikana na madiwa wa kata nyingine pamoja na  mbunge wa Kawe kuleta maendeleo katika Jimbo la Kawe”, alisema Mashaga.

Rwakatale amechaguliwa baada ya kuwashinda vigogo waliogombea nafasi  hiyo  kama alivyokuwa meya wa  manispaa ya Kinondoni kwa miaka  kumi mh. Salum Londa.

Mashaga alisema kuwa endapo Rwakatale atapata ridhaa ya wananchi kwa kushirikiana na madiwani wenzake watasaidia kuinua michezo kwenye jiji la Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment