AWADHI AWAPA RAHA MASHABIKI WA SIMBA
BAO la dakika ya 90 la Awadh Juma liliwezesha Simba
kuibuka na pointi tatu kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya SC Villa
ya Uganda uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, wakati wa
maadhimisho ya Simba Day.
Awadh
ambaye aliingia kwenye mchezo huo akitokea benchi kuchukua nafasi ya Justuce Majivba alifunga
bao hilo kwa shuti baada ya kutokea piga nikupige kwenye lango la Villa.
Ushindi
huo umenogesha tamasha hilo la Simba Day ambalo hufanyika kila mwaka kabla ya
kuanza kwa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Tamasha
hilo pia lilitumika kuwatambulisha wachezaji wapya wa Simba ambao wamesajiliwa
msimu huu kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu.
Katika
mchezo huo, Simba ilianza kwa kulishambulia lango la Villa, lakini umakini wa
mabeki wake waliweza kuzuia mashambulizi langoni mwao na hivyo kuufanya mchezo
huo kusubiri hadi dakika ya 90 kuweza kubadilisha matokeo ya suluhu.
Wachezaji
wapya waliotambulishwa kwenye mchezo huo ni pamoja na Emery Nimubona, Justice Majivba, Hamis Kiiza na Mwinyi Kazimoto ambaye awali
aliichezea timu hiyo kabla ya kutimkia Uarabuni kucheza soka la kulipwa.
Tamasha
hilo lilinogeshwa na burudani mbalimbali, ambapo awali ulianza mchezo kati ya
viongozi wa Simba na wasanii wa Bongo fleva na Bongo muvi ambao ni mashabiki wa
Simba.
Kwenye
mchezo huo, viongozi wa Simba waliibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na
kocha, Dylan Kerr.
No comments:
Post a Comment