WAWAKILISHI
wa Tanzania katika michuano ya Helsinki Cup 2015, timu ya FC Vito Kilwa kutoka
Kilwa mkoani Lindi,kesho wataanza harakati za kuwania ubingwa wa
michuano hiyo, inayoanza kesho na kumalizika Julai 10, jijini Helsinki nchini
Finland.
Kwa mujibu
wa ratiba iliyotolewa na waratibu wa michuano hiyo, FC Vito Kilwa wanakata
utepe saa 8 mchana kwa saa za Finland dhidi ya na FC Reipas ya Oranssi, kwenye
Uwanja wa 9A Käpylä, kabla ya Jumatatu kucheza na Halikko United uwanjani hapo.
Katika mechi
ya tatu kwenye michuano hiyo, jioni ya kesho Jumatatu FC Vito Kilwa watashuka
tena kwenye dimba la 9B Käpylä, ambako watachuana na NJS ya Keltainen, kisha
Jumanne asubuhi itawavaa Euran Pallo kwenye Uwanja wa 15B Lauttasaari.
FC Vito ambao wako mashindanoni wakiwa na
kikosi cha wachezaji 12, watashuka tena dimbani Jumanne saa 5 asubuhi kukipiga
na HJK ya Kannelmäki Sininen, mechi itakayochezwa kwenye Uwanja wa 15A
Lauttasaari.
Akizungumzia
ratiba hiyo, Mkurugenzi wa Taasisi isiyo ya Kiserikali ya Sports Development
Aid (SDA), ambayo inaimiliki FC Vito kwa ushirikiano na Liike Finland ya
Finland, Chigogolo Mohamed, alisema wameipokea kwa mikono miwili na wako fiti
kuikabili.
Wachezaji wa
FC Vito iliyoagwa jijini Dar es Salaam na Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF), Boniface Wambura, ni Charles Fulco, Hussein Bandari, Hussein
Hassani, Shabani Mpogolo, Rashidi Masimba na Hassani Salum.
Wengine ni Yahaya
Ruambo, Alex Muhando, Shabani Kikali, Twahir Ismail, Arafat Babu na Ahmad
Kokolo, ambao wako chini ya kocha Mohamed Mtule na Mkuu wa Msafara (H.O.D), ni
Chigogolo.
Helsinki Cup ni michuano ya nne kwa ukubwa
miongoni mwa mashindano ya vijana barani Ulaya na mwaka huu inashirikisha zaidi
ya timu 1,200, ambayo itafikia tamati Julai 10 kwenye viwanja
mbalimbali jijini Helsinki, nchini Finland.
No comments:
Post a Comment