Pages

Friday, July 17, 2015

VAN GAAL AWATAKA WACHEZAJI WAPYA WAJITUME UWANJANI

Meneja wa Manchester United Louis van Gaal amesema Kipa Victor Valdes atauzwa baada ya kugoma kuidakia Timu yao ya Rizevu. Meneja wa Manchester United Louis van Gaal amesisitiza Viungo wake wapya hawahakikishiwi namba kila Wiki Timu yao ikicheza Msimu mpya ukianza na wanaapaswa kupigania namba zao.
Viungo hao wapya, Morgan Schneiderlin na Bastian Schweinsteiger, wamenunuliwa hivi Juzi kwa Dau la Pauni Milioni 40 na wameungana na wapya wengine Memphis Depay na Matteo Darmian.
Akiongea kabla ya Man United kucheza Mechi yao ya kwanza huko Seattle, Marekani Jumamosi Asubuhi dhidi ya Klabu ya Mexico Club America, Van Gaal amesema Schneiderlin na Schweinsteiger inabidi wakaze buti kuwapiku
Michael Carrick na Daley Blind ili kupata namba.
Van Gaal, akikumbushia Msemo wake wa Msimu uliopita kuwa Kikosi chake hakina uwiano Uwanjani na kusisitiza sasa amepata Viungo imara, pia alifafanua: "Katika Michezo ya juu, hata nafasi yangu haina uhakika. Hata Wachezaji pia, wanapaswa kupigana. Morgan Schneiderlin anapaswa kupigana na Schweinsteiger, Michael Carrick, Daley Blind, hawa ndio Wachezaji wanaoweza kucheza Kiungo katikati."
Aliongeza: " Matteo Darmian inabidi apigane na Valencia, wote wanajua hilo. Michael Carrick anajua hilo, nlimwambia mwishoni mwa Msimu uliopita."
Kuhusu Wachezaji wake wapya, Van Gaal ametoboa kuwa Schneiderlin ndio yuko kwenye nafasi nzuri kutinga moja kwa moja Kikosi cha Kwanza kutokana na uzoefu wake wa kucheza Ligi Kuu England kwani alikuwa huko Southampton.

No comments:

Post a Comment