Pages

Saturday, July 4, 2015

SIMBA NA AZAM WAFANYA MAZOEZI KIWANJA KIMOJA LEO






KATIKA hali ambayo ni nadra kutokea timu za Simba na Azam FC, leo zimejikuta  zikikutana kwenye ufukwe wa Coco jijini Dar es Salaam.
Azam FC ambao wananolewa na Stewart Hall ndio walikuwa wa kwanza kufika eneo hilo na kuanza mazoezi kama programu ya kocha ilivyopanga na baadae Simba nayo iliwasili eneo hilo na kuanza mazoezi chini ya kocha wao mwingereza Dylan Kerr.
Azam walikuwa upande wa kushoto wakifanya mazoezi ya stamina huku Simba wao walikaa kulia na kuanza mazoezi yao lakini kutokana na ufinyu wa eneo Simba walilazimika kukimbia na kupita eneo ambalo Azam walikuwa wakifanya na kuwafanya wachezaji kuanza kutaniana maana wote walikuwa wakikimbia kuelekea upande mmoja lakini Simba walienda mbali zaidi ya Azam.
Kocha Kerr  alikuwa akiongoza mazoezi kwa vitendo alisikika akiwaambia kuwa waweke mawazo yao kwenye Simba na siyo kufikiria Azam, Yanga au Ruvu shooting bali ni Simba kwanza.
Zoezi la Simba kuendelea kufanya mazoezi kupita eneo ambalo Azam FC walipo na sasa ikamfanya Mgosi kujisahau na kuanza kupiga stori na mchezaji wa Azam FC hadi alipoitwa na kocha Matola kwani kocha alikuwa bado anaendelea na program ya mazoezi
Wakati Simba na Azam FC wakiwa Coco, wapinzani wao Yanga wao walikuwa Ufukwe wa Gymkhana wakifanya mazoezi.
Simba inayonolewa na Dylan Kerr inajiandaa na ligi kuu inayotarajiwa kuanza Agosti 22 wakati Azam na Yanga wao wanajiandaa na mashindano ya Kagame yanayotarajiwa kuanza Julai 18 jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment