Serena Williams akipozi na kivazi chake. |
LONDON, England
BAADA ya kushinda mataji ya tenisi ya
Wimbledon, bingwa kwa upande wa wanawake Sereina Williams na Novak Djokovic kwa
wanaume, jioni ya jana walitinga katia pati wakiwa na vivazi tofauti na vile
walivyozoeleka kuonekana navyo uwanjani.
Katika pati hiyo kubwa bingwa mtetezi Novak
Djokovic aliyemshinda bingwa mara saba Roger Federer, alitinga akiwa amevali
suti huku Williams gauli refu `maksi’langi ya maziwa.
Hilo ni taji la tatu la mashindano ya
Wimbledon na ni la tisa kubwa kwa Djokovic wakati Serena akiweka rekodi ya kuwa
mchezaji wa kwanza mwenye umri mkubwa kutwaa taji la mashindano makubwa kwa
upande wa wanawake.
Williams alitimixza miaka 33 na takribani
siku 289 Jumamosi wakati akimfunga Garbine Muguruza wa Hispania kwa seti 6-4,
6-4 na kukamilisha taj lake la 21 kwa mchezaji mmoja mmoja na kujiweka vizuri
kumaliza kalenda ya mashindano makubwa vizuri wakati atakaposhiriki US Open.
Serena Williams. |
Serena Williams (kushoto) na Novak Djokovic |
Wakali hao wakiwa na mataji hayo wakati wa pati hiyo ya ushindi. |
Serena Williams katika kivazi alichozoeleka kuonekana nacho. |
No comments:
Post a Comment