LONDON, England
RAHEEM Sterling amekamilisha
uhamisho wake kwenda Manchester City wa kitita cha pauni milioni 49 huku yeye
akiondoka na pauni 180,000 kwa wiki kama mshahara wake.
Mchezaji huyo ambaye
alipokuwa Liverpool alikuwa akilipwa chini ya pauni 80,000 na baadae kuahidiwa kuongezwa
hadi 100,000 kama angeendelea kuitumikia timu hiyo, aligoma kubaki Anfield.
Raheem Sterlin akiwa na timu ya watoto wenye umri chini ya miaka mitano ya Man City. |
Mwakilishi wa Sterling, Aidy Ward alizungumza
hadharani kuwa mchezaji huyo hakuwa na furaha hapo Anfield wakati wakielekea
mwishoni mwa msimu uliopita, ambapo alisema kuwa mcheaji wake hata akiongezwa
pauni 900,000 kwa wiki, hatabaki Liverpool.
Ward pia alidai kuwa kiungo
huyo hakuwa na uhusiano mzuri na kocha wake Brendan Rodgers, lakini madai hayo
yalikanushwa na kocha huyo wa Liverpool.
Lakini kufuatia vipimo vya
afya katika klabu ya Man City, Sterling aliuambia mtandao wa klabu hiyo: ‘Napenda
kuwashukuru watu wote wanaonizunguka, mama yangu na dada zangu, uongozi wa timu,
na Aidy Ward kwa kunisaidia na kufika nilipo leo.
Nimefurahi kwa mambo yote
kukamilika.’
Sterling mwenye umri wa
miaka 20, aliweka wazi nusu ya pili ya msimu kuwa, hana mpango wa kuongeza
mkataba Liverpool na katika mahojiano katika televisheni Aprili mwaka huu kuwa
kinachomuondoa Liverpool sio pesa.
Laklini, baada ya
kukamilisha kuondoka Liverpool, Sterling ametumia muda wake kumpongeza Rodgers.
‘Napenda kumshukuru Rafa Benitez kwa
kunipeleka Liverpool wakati nikiwa na umri wa miaka 15 na Kenny
Dalglish for kwa kuonesha imani kwangu wakati nikiwa na umri mdogo.
‘Mwisho napenda
kumshukuru Brendan Rodgers kwa kunipatia nafasi ya kudumu katika timu ya kwanza
na kukionesha duniani kipaji changu.’
Sterling, atakayevalia jezi
namba 7 katika timu hiyo yenye maskani yake kwenye uwanja wa Etihad na kufuzu
vipimo vya afya kabla yakusaini mkataba mpya ambao utamuwezesha kuondoka na
pauni 180,000 kwa wiki, alisema anaangalia mbele kukutana na wachezaji wenzake
wapya.
Mchezaji huyo alikiri kuwa
alizungumza na kipa Joe Hart kuhusu kuhamia katika klabu hiyo wakati
walipokutana katika timu ya taifa ya England.
No comments:
Post a Comment