Pages

Saturday, July 4, 2015

NI PATASHIKA LEO FAINALI YA COPA AMERICA CHILE vs ARGENTINA SAA 5:00 USIKU

Leo Argentina watatinga ndani ya Estadio Nacional de Chile Jijini Santiago kuwavaa Wenyeji Chile katika Fainali ya Copa America wao wakisaka Taji la kwanza baada ya Miaka 22 wakati Chile wakitaka kubeba Kombe lao la kwanza katika Historia yao.Nchi hizi Majirani huko Marekani ya Kusini zimeshakutana mara 36 katika Mechi rasmi za Mashindano na Chile kushinda mara 1 tu, Mechi ya Mchujo ya Kombe la Dunia Mwaka 2008 Mjini Santiago, wakati kwenye Mechi za Copa America, Chile hawajaishinda Argentina hata mara moja katika Mechi 24 walizokutana.Ikiwa Argentina watatwaa Copa America hiyo Jumamosi watafungana na Uruguay, Nchi iliyolitwaa mara nyingi kupita yeyote, kwa wote kulitwaa mara 15.
Chile, katika Mashindano 36 ya Copa America, wamefika Fainali mara 4 na zote kupigwa na kulikosa Kombe.
Kwa Lionel Messi, Kepteni wa Argentina ambae amewahi kuwa Mchezaji Bora Duniani mara 4, hii ni nafasi murua kutwaa Taji kwa mara ya kwanza akiwa na Timu ya Kwanza ya Nchi yake ili kuwa na mafanikio kama yale ayapatayo akiwa na Klabu yake FC Barcelona ya Spain. 
Angel D Maria aanza kuonesha makali yake sasa!
Mataji pekee ambayo Messi ametwaa akiwa na Argentina ni yale ya Timu za Vijana za U-20 kwenye Michezo ya Olimpiki.
Kwenye Fainali hii, Argentina itaingia ikiwa na Kikosi kamili wakati Chile itamkosa Sentahafu wao Gonzalo Jara ambae amefungiwa Mechi 3 baada ya kunaswa akimsakama Dole makalioni Straika wa Uruguay Edinson Cavani kwenye Mechi ya Robo Fainali.

Fainali hii inazikutanisha Timu zilizofunga Bao nyingi kwenye Mashindano haya ambapo Chile, chini ya Kocha toka Argentina Jorge Sampaoli, imepiga Bao 13 na Argentina, chini ya Kocha Gerardo 'Tata' Martino, imefunga Bao 10 na 6 zikiwa kwenye Mechi moja tu walipoinyuka Paraguay 6-1 kwenye Nusu Fainali.
Takwimu inayogusa wengi ni ile ya Lionel Messi kufunga Bao 1 tu katika Mechi 5 za Mashindano haya, tena Bao la Penati, lakini hilo halimkeri Tata ambae amesema ni sawa tu mradi Messi acheze vyema na asaidie wengine kufunga. 

Jorge Sampaoli

No comments:

Post a Comment