LOUIS VAN GAAL ASEMA MASTRAIKA WANATOSHA KWA SASA
Kocha
mkuu wa Manchester United Louis Van Gaal ametamba kuwa hatanunua
mshambuliaji mwingine kwani alio nao kwa sasa wanatosha wakiongozwa na
Wayne Rooney.
Pamoja na Wayne Rooney washambuliaji wengine waliobaki
ni Javier Hernandes Chicharito, na James Wilson baada ya mshambuliaji
mpachika magoli Robin Van Persie kujiunga na Fenerbahce ya Uturuki hivi
karibuni na Radamel Falcao mkopo wake kumalizika.
Van
Gaal anatarajia kumtumia Rooney kama mshambuliaji pekee pale mbele
ambapo atasaidiwa na Mephis Depay aliyesajiliwa wakati wa majira ya joto
kutoka PSV Eindhovenya Uholanzi.
Van Gaal anatamba kuwa Depay anaweza kuwa mshambuliaji wa katikati tofauti na alivyokuwa akitumika wakati alipokuwa PSV.
No comments:
Post a Comment