Pages

Saturday, July 4, 2015

AZAM TV KUONYESHA ‘LIVE’ LIGI KUU ENGLAND KWA KISWAHILI

Dar es Salaam MAMBO yakienda vizuri, Azam TV itakuwa kituo cha kwanza cha runinga nchini kurusha ‘live’ mechi za Ligi Kuu England kwa Lugha ya Kiswahili. 
Hadi sasa uongozi wa Azam TV upo kwenye mipango ya kuhakikisha unarusha ligi hiyo ‘live’ kutoka England katika msimu ujao unaotarajiwa kuanza mapema mwezi ujao. Akizungumza na Championi Jumamosi, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media, Tido Mhando, alisema wamejipanga kuhakikisha wanalikamilisha hilo mapema.

No comments:

Post a Comment