HUKU
ikishuhudiwa na wachezaji na wachezaji wake wa kigeni Donaldo Ngoma na Joseph
Tetteh Zutah waliowasili Dar es Salaam leo, Yanga ilijukuta ikitoka sare ya
bila kufunga na Sports Club Villa ya Uganda kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa
kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kwenye mechi
hiyo maalumu kwa ajili ya kupinga mauji ya albino na mgeni rasmi kuwa Mkuu wa
Mkoa wa Dar es Salaam Saidi Mecky Sadiki, Yanga ilipoteza nafasi nyingi za
kufunga kwenye mchezo huo.
Washambuliaji
wa Yanga wakiongozwa na Amisi Tambwe na Simon Msuva walishindwa kufurukuta
mbele ya ukuta thabiti wa Sports Club Villa ambao ni mabingwa wa Uganda.
Yanga
iliwachezesha wachezaji wake wapya iliowasajili msimu huu kama vile winga Deus
Kaseke aliyetoka Mbeya City, Malimi Busungu aliyetoka Mgambo JKT na chipukizi
Godfrey Mwashuiya aliyesajiliwa wakati wa dirisha dogo walishindwa kabisa
kuipenya na kushuhudia wakipoteza nafasi kadhaa za kufunga hasa kipindi cha
kwanza.
Malimi
Busungu alikosa bao la wazi kwenye dakika ya 31 baada ya kupokea pasi nzuri ya
winga Goefrey Mwashuiya, lakini mpira aliopiga ulitoka pembeni kidogo ya Yanga
la Sports Club Villa na dakika ya 39 Amis Tambwe alikosa bao la wazi akiwa
ambeki peke yake na kipa wa Villa Sebweto Nicholaus.
Kwenye mechi
hiyo timu zote zilifanya mabadiliko kadhaa kwa Yanga kuwapumzisha Malimi
Busungu na kumuingiza Kpah Sherman na Nadir Haroub’Cannavaro’ alitoka baada ya
kuumia na kuingia Pato Ngonyani.
Huku Villa
ikiwatoa Kasule Abdulkarim na kumuingiza Dua Abeid na kisha kumtoa Kazibente
James na kumuingiza Kamazi Dennis.
Hata hivyo
Yanga walipata penalti kwenye dakika ya 79 baada ya Deus Kaseke kuangushwa
kwenye eneo la hatari lakini Simon Msuva alipaisha penalti hiyo na kuinyima
Yanga ushindi kwenye mechi hiyo ya kujipima nguvu kujiandaa na mashindano ya
kombe la Kagame.
Yanga mpaka
sasa imecheza michezo miwili ya kujipima nguvu ambapo wiki hii iliifunga klabu
ya daraja la kwanza ya Friends Rangers kwa mabao 3-2 kwenye mechi iliyochezwa
kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.
No comments:
Post a Comment