Pages

Wednesday, June 3, 2015

Wadhamini waunga mkono hatua ya Blatter

Rais wa shirikisho la soka duniani Sepp Blatter
Wadhamini wakuu wa FIFA wameafiki tangazo la Bwana Blatter kujiuzulu, wakisema kuwa ni hatua bora kuelekea mageuzi ya shirikisho hilo.
Kampuni ya Coca-Cola inasema inaamini kuwa uamuzi huo utaisaidia FIFA kuchukua hatua za dharura kushughulikia masuala yaliyoibuka .
Wakuu wa soka barani Ulaya pia wameridhishwa na uamuzi huo.
Wakati huo huo Mwanamfalme wa Jordan Ali bin al Hussein aliyeshindwa katika uchaguzi wa rais wa FIFA wiki iliyopita ameashiria kuwa anaweza kujiandaa tena kuwania nafasi hiyo.

No comments:

Post a Comment