Pages

Saturday, June 6, 2015

UEFA CHAMPIONS LEAGUE: FAINALI NI LEO KATI YA JUVENTUS vs BARCELONA NANI KUIBUKA KIDEDEA????


Leo huko Berlin, Germany, ni Fainali ya UEFA CHAMPIONS LIGI ambayo FC Barcelona ya Spain na Juventus ya Italy zitacheza na hii, kwa kila moja, ni Fainali yake ya 8.
Timu yeyote itakayotwaa Ubingwa huu wa Ulaya hii Leo itakuwa imetwaa Trebo Msimu huu baada ya Timu zote mbili kutwaa Makombe mawili Nchini mwao yale ya Ubingwa na Kombe la Nchi.
Habari kubwa ya Fainali hii ni kukosekana kwa ule mvuto mkubwa wa kuwakutanisha tena kwa mara ya kwanza Beki wa Juventus Giorgio Chiellini na Fowadi wa Barcelona Luis Suarez baada ya Chiellini kuumia Jumatano.

Wachezaji hao walivaana huko Brazil Mwaka Jana wakizichezea Nchi zao kwenye Fainali za Kombe la Dunia na Suarez kuadhibiwa kwa Kifungo kirefu kwa kumng'ata Meno Chiellini.
Lakini kila Timu ina Kikosi thabiti kwa Barca kuongozwa na Mashambulizi ya Mtu 3 ya Lionel Messi, Neymar na Luis Suarez ambao Msimu huu wamefunga zaidi ya Jumla ya Mabao 120 wakati Kikosi kizima cha Juventus kimefunga Bao 105 tu.
Hata hivyo, Juve, wakiongozwa na Wakongwe Kipa Buffon na Kiungo Andrea Pirlo ni Timu yenye uzoefu huku mashambulizi yao yakipambwa na Muargentina Carlos Tevfez, ambae Lionel Messi ametahadharisha ni hatari, akiwa pamoja na Mchezaji wa zamani wa Real Madrid Alvaro Morata wakisaidiwa na Arturo Vidal kutoka Chile.

No comments:

Post a Comment