Pages

Saturday, June 6, 2015

TOM CLEVERLEY KUJIUNGA NA EVERTON

Kiungo Tom Cleverley atajiunga na Everton Julai 1 wakati Mkataba wake na Manchester United utakapomalizika.
Msimu uliopita Cleverley aliichezea Aston Villa kwa Mkopo na kuisaidia kuifikisha Fainali ya FA CUP ambayo ilifungwa na Arsenal.
Everton imempa Mkataba wa Miaka Mitano kuanzia hiyo Julai 1.
Ijumaa Cleverley aliitwa kwenye Kikosi cha England kumbadili Mchezaji wa Tottenham Hotspur, Ryan Mason, ambae ameumia.
England itacheza Mechi ya Kirafiki na Ireland hapo Jumapili na kisha Wiki ijayo kucheza na Slovenia kwenye Mechi ya Kundi lao la EURO 2016.
Meneja wa Everton, Roberto Martinez, akiongea kwenye Tovuti ya Klabu hiyo amesema Cleverley ni fiti kucheza Timu yao na ni mzoefu wa Ligi Kuu England.
Akiwa na Man United, Cleverley alitwaa Ubingwa wa Ligi Kuu England Mwaka 2013 lakini alishindwa kupata namba ya kudumu katika Timu ya na aliwahi kupelekwa kucheza kwa Mkopo huko Leicester City, Watford, Wigan Athletic na kumalizia na Villa.

No comments:

Post a Comment