Waziri mkuu nchini Morocco Abdelilah Benkirane ameamrisha kufanywa
uchunguzi kuhusu matangazo ya runinga ya tamasha ya mwanamuziki Jennifer
Lopez.
Tamasha hiyo inayofahamika kama Mawazine iliandaliwa mjini
Rabat tarehe 29 mwezi Mei na kupeperushwa na kituo cha runinga cha 2M.Bwana Benkirane amesema picha kutoka kwa tamasha hilo zilikuwa potovu na kuongeza kuwa matangazo hayo yalikiuka sheria za matangazo ya picha za nchi hiyo.
Wiki iliyopita waziri wa mawasiliano nchini Morocco alilaumiwa kwa kuruhusu tamasha hilo kupeperuswa kupitia runinga ya taifa hali iliyobabisha kuwepo wito wa kumtaka ajiuzulu.
Akimuandikia barua rais wa halmashauri ya matangazo ya redio na runinga nchini Morocco , bwana Benkirane alitaka halmashauri hiyo kuwachukulia hatua za kisheria wale waliohusika.
Alisema kuwa wale wanaosimamia shirika hilo la utangazaji walishindwa kuingilia kati na kuzuia kutangazwa kwa picha potovu. Lopez amefanya tamasha nchini Morocco awali bila kuwepo tatizo lolote , lakini hii ndiyo mara ya kwanza moja ya tamasha zake zimepeperushwa kwa njia ya runinga.
Nalo kundi linalohusika na elimu la TMZ linasema kuwa linamshtaki mwimbaji huyo kwa kuwa Lopez ameshusha hadhi ya wanawake.
No comments:
Post a Comment