Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro, leo kimeendelea na mazoezi asubuhi na jioni katika uwanja wa Benki ya Biashara ya Ethiopia kujiandaa na mchezo dhidi ya Misri.
Jana
kikosi cha Stars kilifanya mazoezi majira ya saa 9 mchana katika uwanja
wa Taifa wa Ethiopia (Addis Ababa) ambao pia unatumiwa na timu yao ya
Taifa kwa mazoezi.
Taifa
Stars ambayo imeweka kambi jijini Addis Ababa nchini Ethiopia
inajiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika
(AFCON) mwaka 2017 dhidi ya timu ya taifa ya Misri.
Daktari
wa Taifa Stars, Billy Haonga amesema hali ya hewa ya Addis Ababa ni
nzuri kwa maandalizi ya mchezo dhidi ya Misri, kutokana na timu kufanya
mazoezi katika ukanda wa juu (mwinuko kutoka usawa wa bahari) hali
itakayopelekea wachezaji kuwa fit kwa ajili ya mchezo.
Hali
ya hewa ya Alexandria ni ya kawaida, hakuna baridi sana kutokana na
kuzungukwa na bahari ya la Mediterania, hivyo kipindi cha wiki moja
tutakachokuwa kambini hapa Addis Ababa tunatarajiwa vijana watakua
vizuri kabisa kw aajili ya mchezo” Alisema Haonga”.
Wachezaji
wote wa Taifa Stars waliopo kambini Addis Ababa wapo katika hali nzuri,
kiafya, kifikra na morali ya juu kujiandaa na mchezo dhidi ya
Mapaharao.
Wenyeji
Chama cha Soka cha Ethiopia (EFF) wanaangalia uwezekano wa Taifa Stars
kupata mchezo mmoja wa kirafiki wa kujipima nguvu kabla ya kuelekea
nchini Misri.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
No comments:
Post a Comment