Pages

Wednesday, June 3, 2015

SEPP BLATTER ATANGAZA KUJIZULU URAIS FIFA.

Sepp Blatter, ambae alikuwa Rais wa FIFA kwa Miaka 17, ametangaza kuwa atajiuzulu wadhifa wake.
Uamuzi huu unafuatia Shirikisho hilo la Soka Duniani kuandamwa na kashfa ya rushwa ambayo ilipamba moto baada ya Marekani kufungua Mashitaka kwa Maafisa kadhaa wa juu wa FIFA.
Blatter amesema ataitisha haraka iwezekanavyo Kongresi ya FIFA ili kuchagua Rais mpya baada ya yeye kukiri hana sapoti ya kila Mtu kufuatia na kusakamwa na Skandali hiyo.
Akitangaza uamuzi huo, Blatter, ambae Ijumaa iliyopita alichaguliwa kwa Kipindi cha 5 cha kuwa tena Rais wa FIFA, alisema: "Nimefikiria sana kuhusu Urais wangu na Miaka 40 ya FIFA katika maisha yangu. Naipenda FIFA kupita kitu chochote na nataka kufanya vyema. Niliamua kusimama tena kupigania Urais kwa nia ya kuleta mambo mapema katika Soka. Lakini uchaguzi wangu unaelekea haungwi mkono na kila Mtu. Ndio maana nitaitisha KIkao cha Dharura ili kunibadili na sitagombea."
Hadi hapo Kikao hicho cha Dharura kitakapofanyika, Tarehe ambayo bado haijulikani, Blatter ataendelea kuwa Rais wa FIFA.
Kikao cha kawaida cha Kongresi ya FIFA kilitarajiwa kufanywa huko Mexico City, Mexico Mwakani Mei 16 lakini Blatter ametoboa hatafika wakati huo.
Sepp Blatter

No comments:

Post a Comment