Pages

Thursday, June 25, 2015

JAMBO BUKOBA KUIWAKILISHA TANZANIA KWENYE KONGAMANO LA MICHEZO LA " DISCOVER FOOTBALL" NCHINI UJERUMANI.

Shirika la Jambo Bukoba limepata Mwaliko kuhudhura Kongamano la Michezo Nchini Ujerumani lenye Malengo ya Kuinua Wanawake kupitia Kwenye Michezo(Soccer). Wakiwa Ughaibuni Ujerumani Watajifunza haki za Wanawake Kiujumla ili wawe Mabalozi kwa wenzao hapa Hapa Nyumbani. Kongamano hilo la Michezo linaloitwa Discover Football litashirikisha Nchi 100 na Tanzania itawakilishwa na Shirika hilo la Jambo Bukoba lenye Maskani yake Mkoa wa Kagera. Safari hiyo itaanza kesho juni 25, 2015. Picha na Faustine Ruta, Bukoba.

Jambo Bukoba ni Shirika lisilokuwa la Serikali linalofanya kazi mkoani Kagera kwa kushirikiana na serikali ya Mkoa.
Mwanzilishi wa Jambo Bukoba ni Bw. Clemence Mlokozi ambaye asili yake ni Mkoani Kagera katika Wilaya ya Missenyi Kijiji Ishozi na anaishi nchini Ujerumani.
Jambo Bukoba ilianzishwa Mkoani Kagera kwa kusaidia watoto hasa wanafunzi wa shule za msingi kuanzia miaka 5 hadi 19 kujenga afya zao kimichezo ili kujikinga na Maabukizi ya UKIMWI, kuweka haki sawa katika elimu kupitia michezo kwa wasichana na wavulana.
Shirika hili chini ya mwanzilishi wake Bw. Mulokozi tangu kuanzishwa kwake mkoani Kagera limekuwa likiwafunza watoto katika shule za msingi kila wilaya michezo midogo midogo ya kujenga ushirikiano wa pamoja hasa watoto wa kike kujiamini na kushirikiana zaidi na wenzao wa kiume.
Kongamano hilo litafanyika katika Mji wa Berlin, Germany kuanzia tarehe 27 juni - 06 julai, 2015 na wawakilishi hao watakaa huko juma moja/ siku saba. Msafara huo Unaongozwa na Gonzaga Stephen ambaye ni Meneja wa Mradi huo wa Jambo Bukoba akisaidiana na msaidizi wake Bi. Imani Paul. Pia watandamana na Walimu mmoja mmoja kwa kila Shule za Msingi baadhi kutoka Kila Wilaya saba. 
Walimu hao ni Peace Saleand kutoka Biharamulo- Rubondo Shule ya Msingi. Grace Wamara kutoka Shule ya Msingi Tumaini ambayo Ipo Bukoba Mjini. Alistidia Bijura kutoka Shule ya msingi Kaisho - Kyerwa.

Elizabeth John kutoka Rulenge Shule msingi - Ngara
Abela Ndeyokobora Kutoka Shule ya Msingi Kayanga - Karagwe
Jeni Mulokozi Kutoka kashekya Shule ya Msingi - Misenyi
William Magosa kutoka Karalo Shule ya Msingi -Karagwe


Kushoto ni Ni Meneja wa Mradi wa Jambo Bukoba Gonzaga Stephen akiwa na Walimu ambao wataiwakilisha Tanzania kupitia Shirika hilo la Jambo Bukoba Huko Berlin Ujerumani hivi karibuni kwenye Viwanja vya Gymkana Bukoba Mjini.
Washiriki ambao wataiwakilisha Tanzania kwenye Kongamano/Tamasha hilo la Michezo la Discover Football, Picha na Faustine Ruta, Bukoba

No comments:

Post a Comment