Pages

Thursday, June 18, 2015

GOLDEN STATE WARRIORS MABINGWA WA NBA


Timu ya Golden State Warriors ndio washindi wa ligi ya mpira wa vikapu nchini Marekani katika kipindi cha miaka 40,baada ya kuishinda Cleveland Cavaliers 105-97 na kuibuka kidedea kwa kushinda misururu 4-2.Stephen Curry na Andre Iguodala,akiwa mchezaji bora katika michuano hiyo alipata pointi 25 kila mmoja.
Nyota wa Cavaliers Lebron James aliiongoza timu yake iliojaa majeruhi baada ya kujipatia pointi 32.''Hiki ni kitu maalum.Kuanzia mwanzo wa msimu huu hiki ndicho tulichotarajia'',alisema Curry. Mchezaji wa Golden State Warriors 
The Warriors walipigiwa upatu kushinda taji hilo baada ya kuwa na rekodi nzuri katika msimu wote na ilikuwa timu ya kwanza baada ya Chicago Bulls mwaka 1991 kushinda taji wakiwa bila wachezaji walio na uzoefu wa kufika fainali ya mashindano hayo.
Steve Kerr alikuwa kocha wa kwanza mpya kushinda taji hilo tangu Pat Riley alipoifunza Los Lakers mwaka 1982.


Mchezaji bora Stephen Curry

No comments:

Post a Comment