Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Monday, June 29, 2015

BRAZIL YAFUNGISHWA VIRAGO NA PARAGUAY COPA AMERICA BAADA YA KUFUNGWA PENATI 4-3

Paraguay wameifunga Brazil usiku huu kwa Mikwaju ya Penati (3-4) kwenye Michezo ya Copa America na Sasa kukutana uso kwa Uso na Argentina Nusu Fainali.Wachezaji wa Brazil wakiwa hoi wakati Mikwaju inamalizika na Paraguay kuibuka Kidedea usiku huu kwenye Mashindano ya Copa America.Robinho akishangilia bao lake la dakika ya 15 kipindi cha kwanza kwa kuipatia bao 1-0 dhidi ya Paraguay baada ya kupata pasi safi kama kona kutoka kwa Dani Alves. 
Mpaka mapumziko Brazil ilikuwa ikiongoza kwa bao 1-0 dhidi ya Paraguay. Derlis González dakika ya 72 kipindi cha pili aliisawazishia bao kwa mkwaju wa penati na mtanange kumalizika dakika 90 kwa 1-1 na Mikwaju kupigwa.
Kocha wa Brazil Dunga amewataka radhi na pole Mashabiki wa Brazil baada ya kutupwa nje.
Matokeo haya yanaifanya Paraguay, kwa mara ya pili mfululizo, kuitoa Brazil kwenye Mashindano haya, kwenye hatua hii hii, kwa Mikwaju ya Penati kwani Mwaka 2011 huko Argentina waliwabwaga Brazil kwa Penati 2-0 baada ya Brazil kukosa Penati zao zote 4.
Paraguay sasa wapo Nusu Fainali na watacheza na Argentina hapo Jumanne wakati Jumatatu ni Nusu Fainali nyingine kati ya Wenyeji Chile na Peru.
Shabiki wa Brazil wakiwa tayari kuangalia kipute!Brazil v Paraguay

No comments:

Post a Comment