Pages

Wednesday, May 27, 2015

DIEGO COSTA NJE KIKOSI CHA SPAIN CHA MECHI ZA JUNI

Kocha wa Spain Vicente del Bosque amewaita Vijana wapya wawili wa Sevilla, Sergio Rico na Aleix Vidal, kwa ajili ya Mechi zao za Juni dhidi ya Costa Rica na Belarus na kumwacha Straika wa Chelsea Diego Costa.Kipa Rico, Miaka 21, na Winga Vidal, Miaka 25, wamekuwa waking'ara Msimu huu na Sevilla ambayo imemaliza La Liga ikiwa Nafasi ya 5 na Jumatano Mei 27 huko Stadion Narodowy Mjini Warsaw, Poland, watacheza na Klabu ya Ukraine Dnipro Dnipropetrovsk kwenye Fainali ya Europa Ligi.

Wachezaji hao wawili wanaungana na mwenzao wa Sevilla, Vitolo, kwenye Kikosi cha Wachezaji 24 wa Spain.
Spain watacheza Mechi ya Kirafiki na Costa Rica huko Jijini Leon, Spain hapo Juni 11 na Juni 14 kucheza Ugenini huko Borisov na Belarus kwenye Mechi ya Kundi lao la EURO 2016.
 
Kocha wa Spain Vicente del Bosque amewaita Vijana wapya wawili wa Sevilla, Sergio Rico na Aleix Vidal, kwa ajili ya Mechi zao za Juni dhidi ya Costa Rica na Belarus na kumwacha Straika wa Chelsea Diego Costa.

KIKOSI KAMILI CHA SPAIN:

Goalkeepers: Iker Casillas (Real Madrid), David De Gea (Manchester United), Sergio Rico (Sevilla).

Defenders: Juanfran (Atletico Madrid), Dani Carvajal (Real Madrid), Sergio Ramos (Real Madrid), Gerard Pique (Barcelona), Marc Bartra (Barcelona), Jordi Alba (Barcelona), Juan Bernat (Bayern Munich), Mikel San Jose (Athletic Bilbao)

Midfielders: Koke (Atletico), Sergio Busquets (Barcelona), David Silva (Manchester City), Isco (Real Madrid), Santi Cazorla (Arsenal), Cesc Fabregas (Chelsea), Andres Iniesta (Barcelona), Pedro Rodriguez (Barcelona), Vitolo (Sevilla), Aleix Vidal (Sevilla)

Forwards: Paco Alcacer (Valencia), Alvaro Morata (Juventus), Nolito (Celta).

No comments:

Post a Comment