DAKTARI MWANAMKE, EVA CARNEIRO WA CHELSEA AKEJELIWA NA MASHABIKI
TUHUMA
nzito zimeibuka huko Uingereza kwamba Mashabiki wa Timu pinzani mara
nyingi huimba maneno ya kashfa ya kumdhalilisha kijinsia Daktari Mkuu wa
Chelsea, Eva Carneiro, ambae ni Mwanamama.
Tuhuma hizi zimeibuliwa
na uchunguzi wa Video za BBC, Shirika la Utangazaji la Uingerea, pamoja
na Mitandao mbalimbali ambayo pia imenukuliwa kumshambulia Refa
Msaidizi, Mshika Kibendera Mwanamama, Helen Byrne.
Matukio
hayo yameifanya FA, Chama cha Soka England, kuwahimiza Mashabiki wa
Soka kutoa Ripoti za Mashambulizi ya Ubaguzi wa Kijinsia huku Klabu ya
Chelsea ikitaka Watu kuacha kashfa hizi za kishenzi.
Msemaji
wa Klabu ya Chelsea amesema: “Suala la Usawa wa Kijinsia tunalichukulia
kwa uzito mkubwa na tunashutuma sana ubaguzi wa aina yeyote ukiwa
pamoja na wa Jinsia!”Shutuma hizi zimeibuka baada ya
Utafiti toka Chombo cha Kupinga Ubaguzi kwenye Soka, Kick It Out,
kutoboa Matukio 13 ya Ubaguzi wa Kijinsia kwenye Viwanja vya Soka vya
Kulipwa na vinginevyo kwa Kipindi cha Agosti hadi Desemba 2014.
No comments:
Post a Comment