Huko Vicente Calderon Jijini Madrid, Wenyeji Atletico Madrid wametinga Robo Fainali kwa Mikwaju ya Penati 3-2 baada ya kufungana Mabao na Bayer Leverkusen 1-1 kwa Mechi mbili.
Leverkusen walishinda kwao Germany 1-0 na Jana Atletico kushinda 1-0 kwa Bao la Dakika ya 27 la Mario Suarez na kudumu hadi Dakika 90 kwisha na hivyo Mechi kwenda Dakika za Nyongeza 30 bila kubadilika.
Ndipo ikaja Mikwaju ya Penati 5 na Atletico kushinda Penati 3- 2 huku Antoine Griezman, Mario Suarez na Fernando Torres wakifunga na Raul na Koke wakikosa kwa upande wa Atletico wakati Leverkusen wafungaji ni Rolfes na Castro na Calhanoglu, Toprat na Stefan Kiesling wakikosa.
Atletico, ambao Msimu uliopita walifungwa Fainali ya Mashindano haya na Real Madrid, sasa wanaingia Droo ya kupanga Mechi za Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONS LIGI itakayofanyika Ijumaa pamoja na A S Monaco, Real Madrid, FC Porto, Bayern Munich na Paris Saint-Germain.
Bao la Atletico Madrid lilifungwa na Mario Suárez dakika ya 27 na mtanange kipindi cha pili muda wa kawaida wa dakika 90 ulimalizika bila ya kufunga na kwa Agg 1-1 na mtanange kwenda kwa dakika 120 kwenye Uwanja wa Estadio Vicente Calderón, Madrid ukiongozwa na Refa N. Rizzoli. Mikwaju ya Penati ilipigwa baada ya kumaliza dakika ya 120 wakiwa na Agg 1-1. Atletico Madrid waliweza kushinda mikwaju ya Penati 3-2.
No comments:
Post a Comment