Pages

Tuesday, January 6, 2015

WAAMUZI WAKABIDHIWA BEJI ZA FIFA


 Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),Jamal Malinzi akizungumza na Waandishi wa Habari pamoja na baadhi ya waamuzi waliopata hadhi ya kuwa waamuzi wenye beji za FIFA katika hafla fupi ya iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karume Mchikichini, Jijini Dar es salaam. Jumla ya waamuzi 11 wamepata Beji ya FIFA mwaka huu na kupelekea idadi ya waamuzi wote nchini wenye Beji hizo kufikia 18.Picha zote na Othman Michuzi.

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),Celestine Mwesigwa akizungumza machache katika hafla hiyo.
 Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),Jamal Malinzi akisisitiza jambo kwa waamuzi waliopata beji za FIFA wakati akiwaonyesha kitabu cha Maadili ya FIFA katika hafla iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karume Mchikichini,Jijini Dar es salaam.
 Kiongozi wa Waamuzi wanaume waliopata Beji ya FIFA,Mujuni Mkongo (kati) akizungumza Waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati akitoa shukrani zake kwa uongozi wa TFF kwa jitihada walizozionyesha mpaka kuwafanikisha wao kupata hadhi hiyo,pia alitoa wito kwa Waamuzi wengine kuipenda kazi yao na wajitume zaidi.Kushoto ni Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),Jamal Malinzi na kulia ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),Celestine Mwesigwa.
 Kiongozi wa Waamuzi wanawake waliopata Beji ya FIFA,Hellen Mduma akizungumza Waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati akitoa shukrani zake kwa niaba ya Waamuzi wenzake.Kushoto ni Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),Jamal Malinzi na kulia ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),Celestine Mwesigwa.
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),Jamal Malinzi akimkabidhi Beji ya FIFA,Mwamuzi Jonesia Rukyaa katika hafla iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karume Mchikichini,Jijini Dar es salaam.
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),Jamal Malinzi akimkabidhi Beji ya FIFA,Mwamuzi Sophia Mtongori katika hafla iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karume Mchikichini,Jijini Dar es salaam.
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),Jamal Malinzi akimkabidhi Beji ya FIFA,Mwamuzi Florentina Zablon katika hafla iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karume Mchikichini,Jijini Dar es salaam.
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),Jamal Malinzi akimkabidhi Beji ya FIFA,Mwamuzi Msaidizi Kudra Omar katika hafla iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karume Mchikichini,Jijini Dar es salaam.
Sehemu ya Waamuzi waliopata Beji ya FIFA
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),Jamal Malinzi akimkabidhi Beji ya FIFA,Mwamuzi Kiongozi Mujuni Nkongo katika hafla iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karume Mchikichini,Jijini Dar es salaam.Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Wamuzi Tanzania,Salim Chama.
Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),Jamal Malinzi akimkabidhi Beji ya FIFA,Mwamuzi Msaidizi, Sudi Lila katika hafla iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karume Mchikichini,Jijini Dar es salaam.Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Wamuzi Tanzania, Salim Chama.
Uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) chini ya Rais Jamal Malinzi ukiwa katika picha ya pamoja na waamuzi hao waliopata Beji ya FIFA.

Wanawake waliopata beji za FIFA ni Jonesia Rukyaa toka Kagera, Florentina Zablon toka Dodoma na Sophia Ismail toka Mara kama waamuzi wa kati huku waamuzi wasaidizi ni Hellen Mduma wa Dar es Salaam, Kudra Omary toka Tanga, Grace Wamala toka Kagera na Dalila Jaffary toka Zanzibar.
Kwa upande wa wanaume ni Israel Mujuni wa Dar es Salaam, Waziri Sheha wa Zanzibar, Martin Saanya wa Morogoro na Mfaume Nassoro wa Zanzibar wamepata beji hizo kama waamuzi wa kati huku Samwel Mpenzu wa Arusha, John Kanyenye wa Mbeya, Frednand Chacha wa Mwanza, Josephat Bulali wa Dar es Salaam, Sudi Lila na Frank Komba wa Pwani wakipata beji hizo kama waamuzi wasaidizi.

No comments:

Post a Comment