Pages

Friday, January 16, 2015

SEPP BLATTER AWAPONGEZA CRISTIANO RONALDO NA JOSE MOURINHO KOCHA

Cristiano Ronaldo ameteuliwa kuwa ndie Mchezaji Bora wa Karne huko Nchini kwao Portugal.
Uteuzi wa Ronaldo umefanywa katika Sherehe za kuadhimisha Miaka 100 ya Shirikisho la Soka la Portugal.
Mourinho (middle) celebrates Chelsea's title win with Frank Lampard (left) and John Terry (right) in May 2005
Meneja wa Chelsea, Jose Mourinho, nae amezoa Tuzo ya Kocha wa Karne kwa Portugal katika Hafla hiyo hiyo iliyofanyika ndani ya Estoril Casino, Kilomita 10 toka Jiji la Lisbon huko Nchini Portugal.

Jose Mourinho akipozi kwenye picha leo wakati wa kuteuliwa kuwa Kocha wa Karne

Mourinho akipata picha huko Quinas de Ouro gala jana leo Alhamisi

Ronaldo, ambae Majuzi alizoa Tuzo ya FIFA Ballon d’Or, ikimaanisha yeye ndie Mchezaji Bora wa Mwaka Duniani huko Zurich, Uswisi, ikiwa ni mara yake ya pili mfululizo na pia mara ya 3 kuitwaa, alifunga Bao 60 katika Mechi 61 kwa Mwaka 2014.
Kwa kuteuliwa kuwa Mchezaji Bora wa Karne, Ronaldo aliwabwaga kwa Kura Malejendari wa Portugal, Eusebio na Luis Figo.

Mwenyewe Ronaldo hakuwepo huko Portugal wakati wa Hafla hiyo kwani alikuwa Kambini na Klabu yake Real Madrid ambayo Usiku huu inacheza Dabi ya Jijini Madrid Uwanjani Santiago Bernabeu, ikiwa ni Marudiano ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya Copa del Rey dhidi ya Atletico Madrid ambao walishinda 2-0 katika Mechi ya kwanza waliyocheza kwao.
Cristiano Ronaldo

No comments:

Post a Comment