Pages

Tuesday, January 6, 2015

KOCHA WA POLISI MARA AJIGAMBA KUIPELEKA TIMU LIGI KUU


Kocha wa Polisi Mara, Henry Mkanwa akionyesha vitu vyake kwa wachezaji walipokuwa wanafanya mazoezi Uwanja wa Karume jijin iDar es Salaam


Kikosi cha Polisi Mara

KOCHA wa Polisi Mara, Henry Mkanwa amejigamba kuipandisha timu yake kucheza Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu ujao.

Mkanwa aliyasema hayo jijini Dar es Salaam ambapo timu yake imeweka kambi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa Januari 7, mjini Morogoro.

“Nimejipanga kuhakikisha timu yangu inapanda kucheza ligi Kuu kwa msimu ujao kwani timu yetu ni nzuri na wachezaji wana morali”, alisema Mkanwa ambaye alishawahi kuchezea Reli ya Morogoro

Pia alisema Polisi kwa sasa ina pointi 18 ipo kwenye nafasi ya tano ikiwa imebakiza michezo saba, mitano ya nyumbani  na miwili ya ugenini  atahakikisha wanashinda michezo yote ili aweze kushika nafasi kati ya nafasi mbili za juu zitakazo mwezesha kucheza Ligi Kuu au hata kupata best looser ambaye ataungana na washindi wawili wa juu kutoka katika kundi ilikufikisha timu tano za kuingia Ligi Kuu.

“Kila kundi zinapita timu mbili na timu moja inaingia kama best looser hivyo nitahakikisha napata nafasi ya kucheza Ligi Kuu kwani timu yangu ni bora na wachezaji wana morali”, alijigamba Mkanwa ambaye kwa sasa ana cheo cha Meja.

Polisi Mara inakabiliwa na mchezo na BurkinaFasso ya Morogoro utakaochezwa kwenye dimba la Jamhuri mjini Morogoro, utakaochezwa Januari 7, mchezo ambao Mkanwa anakiri kuwa utakuwa mwepesi kwao kwani wamejiandaa vema ndio maana wameweka kambi jijini Dar es Salaam.

Pia Mkanwa alitoa shukrani kwa wasaidizi wake Clement Kajeli na Omar Hamis na uongozi wa jeshi la Polisi kwa ushirikiano wanaompa kwani unafanya majukumu yake kwenda vema bila vipingamizi.

No comments:

Post a Comment