Pages

Thursday, January 22, 2015

KAGERA WATUPWA NJE YA MASHINDANO YA WANAWAKE TAIFA CUP KWA MATUTA 4-3 NA TIMU YA MWANZA

Na Faustine Ruta, Mwanza
Timu ya Wanawake kutoka Mkoa wa Kagera imetupwa nje ya Mashindano hayo leo kwenye Matuta baada ya kumaliza mtanange wao kwa sare ya Nyumbani Ushindi wa 2-1 na leo Ugenini CCM Kirumba Mwanza 2-1 na Matuta kupigwa na Timu ya Mwanza kuibuka na Ushindi wa bao 4-3. Mchezo huo uliochezwa katika Uwanja wa CCM Kirumba Timu ya Mwanza ndio walianza kupata bao mapema dakika ya 2 kupitia kwa mchezaji wao matata aliyekuwa amevaa jezi no.10 Meriam Kimbuya kwa kukatika katikati ya mabeki na kufunga bao hilo la kwanza. Kipindi cha pili mchezaji huyo huyo Meriam Kimbuya aliwafungia bao tena Mwanza katika dakika ya 64 na kufanya 2-0 dhidi ya timu ya Kagera. Kagera waliongeza Bidii nao dakika ya 73 Mchezaji Anna Katunzi aliachia shuti kali lililomzidi nguvu kipa wa Mwanza na kuishilia nyavuni na kufanya 2-1.
Wachezaji wa Timu ya Wanawake ya Hapa jijini Mwanza wakishangilia baada ya kuifunga Timu ya Kagera kwa matuta. Mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza leo Mchana kwenye raundi ya hatua ya 16 Bora.Raha ya Ushindi!!Mchezaji wa Timu ya Mwanza Meriam Kimbuya akishangilia  bao lake la dakika ya 2
Baadhi ya Viongozi wa Timu ya Kagera wakitoka kwenye Uwanja wa CCM Kirumba leo baada ya kukubali kwa kutoka nje kwa hatua ya Mikwaju ya Penati baada ya kumalizika kwa dakika 90 kwa 2-1 dhidi ya timu ya Mwanza. Katika Mechi ya kwanza Kagera waliwafunga bao 2-1 Timu ya Mwanza hivyo kutokana na matokeo ya leo tena Katika Uwanja wa CCM kirumba kuamua Mwanza kusonga hatua inayofuata ambapo watasafiri Jijini Dar es Salaam. Picha na Faustine wa www.bukobasports.com

Kwenye kasi...... Mchezaji wa Kagera akiambaa na mpira
Kipa wa  timu ya Mwana akiwapanga Wachezaji wakati wa kupiga mpira wa adhabu langoni mwake kipindi cha Kwanza. Picha na Faustine wa www.bukobasports.com
Nani zaidi!! Mahesabu ya kumtoka Mtu yanatakiwa hapa!!
Mchezaji wa Kagera akimpanga mchezaji wa Mwanza kutaka kumzunguka na mpira!Katikati ni Kiongozi Bi. Rukia Kassim Mawenya kwa makini akiangalia Timu ya Kagera kwenye mtanange wa raundi ya 16 bora marudiano
Patashika!
Waamuzi na Timu kepteni kwenye Picha ya pamoja
Kikosi cha Timu ya Kagera kilichoanza.
Wachezaji wawili wa Mwanza wakimlinda mchezaji wa Kagera
Chini ya Ulinzi mkali!Mwamuzi wa kati wa Mtanange huo alimaliza dakika 90 za mchezo na mpira kwenda kwenye hatua ya Matuta baada ya kukomaliana sare Nyumbani na Ugenini bao la Nyumbani likiwabeba Kagera. Picha na Faustine wa www.bukobasports.com
Kikosi cha Timu ya Mwanza kwenye picha ya pamoja na Kocha wao baada ya Mtanange kumalizika
Tunaenda Robo fainali Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment