Pages

Friday, January 16, 2015

ANGEL DI MARIA AJIKOSHA KUWEMO KIKOSI BORA DUNIANI

MCHEZAJI wa Manchester United Angel Di Maria amesema ni heshima kubwa kwake kuteuliwa kwenye Kikosi Bora Duniani, FIFPro World XI, wakati wa Hafla ya Ballon d’Or iliyofanyika Jumatatu Usiku Mjini Zurich Nchini Uswisi.
Di Maria alihudhuria Hafla hiyo na alimshuhudia Mchezaji aliekuwa nae Real Madrid kabla kuhamia Man United, Cristiano Ronaldo, akizoa Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani, FIFA Ballon d’Or, kwa mara ya pili mfululizo.
Uteuzi wa Di Maria kwenye Kikosi cha Wachezaji 11 wa FIFPro World XI ulifanywa kwenye Kura iliyopigwa na zaidi ya Wachezaji 20,000 Duniani kote ambao ni Wanachama wa FIFPro, Chama cha Kutetea Haki za Wachezaji wa Kulipwa Duniani.

Akiongea na Mtandao wa Klabu yake Man United, Di Maria alisema: “Ni heshima kubwa kuwemo FIFPro World XI, kuwemo pamoja na Wachezaji Bora Duniani. Tangu nipo mtoto, Siku zote niltaka kucheza Soka tu na kupata Tuzo kama hii ni bonasi. Ulikuwa Usiku mzuri na namshukuru kila alienichagua!”

Kwa Mwaka 2014, Ange Di Maria, mwenye Miaka 26, aliisaidia Real Madrid kutwaa La Decima, kama wanavyoita kubeba Ubingwa wa UEFA CHAMPIONZ LIGI kwa mara ya 10, na kisha kuibeba Nchi yake Argentina kufanya vyema kwenye Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil na kuifikisha Fainali waliyofungwa na Germany.

FIFA/FIFPro World XI 
Kikosi Bora cha Mwaka
Kipa: Manuel Neuer (Germany/Bayern Munich),

Mabeki: Sergio Ramos (Spain/Real Madrid), David Luiz (Brazil/PSG), Philipp Lahm (Germany/Bayern Munich), Thiago Silva (Brazil/PSG),
Viungo: Andres Iniesta (Spain/Barcelona), Toni Kroos (Germany/Real Madrid), Angel Di Maria (Argentina/Manchester United)
Mafowadi: Arjen Robben (Netherlands/Bayern Munich), Lionel Messi (Argentina/Barcelona), Cristiano Ronaldo (Portugal/Real Madrid).

No comments:

Post a Comment