Pages

Tuesday, December 30, 2014

VAN GAAL ATETEA UCHOVU WA KIKOSI CHAKE KILICHOSHINDWA KUTAMBA WHITE HART LANE

Mechi ya Manchester United walipotoka Sare 0-0 na Tottenham Hotspur Jumapili, Meneja wa Klabu hiyo Louis van Gaal alifafanua uamuzi wake ulitokana na uchovu na si kiwango hafifu huku akidokeza kurudi kadhaa kwa majeruhi kadhaa kundini.
Kwenye Mechi hiyo iliyochezwa White Hart Lane, Van Gaal alimuingiza Rafael kumbadili Antonio Valencia wakati wa Haftaimu na kisha kuwatoa Jonny Evans na Paddy McNair na kuwaingiza Chris Smalling na Luke Shaw ambao walitoka kwenye Listi ya Majeruhi.
Akiongea na MUTV, Kituo cha TV cha Man United, Van Gaal alisema: “Nilifanya mabadiliko hayo ni sababu ya uchovu na si kiuchezaji. Wachezaji walichoka kwa sababu ya kucheza mara mbili ndani ya Saa 48. Kisayansi, mwili hauwezi kuwa kwenye hali nzuri ndani ya Siku 2 na hilo tumeliona Leo.”
Hata hivyo, licha ya kucheza Mechi 2 ndani ya Siku 2, Van Gaal alianzisha Kikosi kile kile katika Mechi hizo mbili na hiyo ikiwa ni mara ya kwanza katika Mechi 85 kwa Man United kuanzisha Wachezaji wale wale katika Mechi mbili mfululizo.
Pia Van Gaal alieleza hali ya majeruhi wako: “Bado tuna Majeruhi Wanne na Marouane Fellaini ni Mgonjwa. Angel Di Maria, Daley Blind, Marcos Rojo na Ander Herrera ni Majeruhi.”
Hata hivyo, Van Gaal alidokeza Herrera atarejea dimbani Wiki hii huku Rojo akikaribia kurudia.

No comments:

Post a Comment