Simon Sserunkuma akitia saini fomu za usajili za Simba baada ya klabu
hiyo kukatisha mikataba ya wachezaji wake wawili wa kimataifa, wote raia
wa Burundi, mshambuliaji Hamis Tambwe na Kiungo Pierre Kwizera, ikiwa
ni siku moja tangu Simba kuifunga Yanga kwenye mchezo wa nani mtani
Jembe.
Beki Juuko Murushid, akitia saini mkataba wa kuichezea Simba. Juuko
aliichezea Simba dhidi ya Yanga katika Uwanja wa Taifa Jijini
Dar-es-Salaam na kuonyesha uwezo mkubwa na kuisaidia Simba kupata
ushindi wa mabao 2-0. Kwa usajili huo, Simba sasa inao wachezaji watano
kutoka Uganda. Wachezaji hao ni George Owino, Emmanuel Okwi, Dan
Sserunkuma, Saimon Sserunkuma na Juuko Murushid
No comments:
Post a Comment