Pages

Friday, December 26, 2014

MECHI YA JKT RUVU, SHOOTING KUCHEZWA USIKU



Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara kati ya JKT Ruvu na Ruvu Shooting itachezwa kesho usiku kwenye Uwanja wa Azam Complex ulioko Chamazi, Dar es Salaam.



Timu hizo zitapambana kuanzia saa 1 kamili usiku katika mechi hiyo itakayoonyeshwa moja kwa moja (live) na Azam Tv.



Viingilio katika mechi hiyo ni sh. 3,000 kwa jukwaa la kawaida na sh. 5,000 kwa upande wa jukwaa la VIP.



Tiketi za kushuhudia mechi hiyo ambazo ni za elektoniki tayari zimeanza kuuzwa kupitia maduka ya Fahari Huduma, M-PESA kwa kupiga *150*03*02# ambayo utapata namba ya kumbukumbu kwa ajili ya kufanya malipo kupitia hiyo hiyo M-PESA na baadaye kuchapa tiketi yako katika mashine maalumu zilizopo kwenye ATM za CRDB.



Pia mshabiki anaweza kununua tiketi kupitia CRDB Simbanking.



Mwamuzi Dominic Nyamisana kutoka Dodoma ndiye atakayechezesha mechi hiyo akisaidiwa na Abdallah Uhako (Arusha), Godwill Kihwili (Arusha) na Hashim Abdallah (Dar es Salaam).



IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

No comments:

Post a Comment