Pages

Wednesday, December 31, 2014

BARCELONA YAWEKEWA PINGAMIZI, HAKUNA KUUZA AU KUNUNUA MCHEZAJI MPAKA MWAKA 2016

BARCELONA haitaruhusiwa kusaini Mchezaji mpya kwa Mwaka wote wa 2015 baada ya Rufaa yao kupinga Adhabu ya FIFA kutupwa nje na CAS [Court of Arbitration for Sport], Mahakama ya Usuluhishi Michezoni.
Awali FIFA iliwafungia Barca kusaini na kuuza Wachezaji baada ya kupatikana na hatia ya kusaini Wachezaji walio chini ya Umri halali kutoka nje ya Spain.
Hii Leo CAS imetoa tamko kuwa Rufaa ya Barcelona kupinga uamuzi wa Kamati ya Rufaa ya FIFA uliotolewa Agosti 19, 2014 ilikuwa haina misingi na ni wazi Klabu hiyo ya Spain ilikiuka Kanuni za FIFA na hivyo watumikie Adhabu kama ilivyoamuliwa na FIFA.
Rufaa hii ya Barca kwa CAS ilitoa mwanya kwao kusajili Wachezaji wapya mara baada ya kuadhibiwa na FIFA na hivyo kumudu kuwanunua pamoja na Luis Suarez, Ivan Rakitic na Alen Halilovic.
Uamuzi huu wa CAS ndio wa mwisho hivyo Barca hawataweza kuingia Sokoni kwenye Madirisha ya Uhamisho ya Januari 2015 na lile la mwishoni mwa Msimu huu.
Pamoja na Adhabu hiyo, Barca pia inatakiwa kulipa Faini ya Euro 375,000.

No comments:

Post a Comment