Pages

Sunday, December 14, 2014

ARUSHA YAFUNGWA NA KINONDONI COPA COCACOLA

Kikosi cha Kinondoni

Kikosi cha Arusha


TIMU ya soka ya mkoa wa Kinondoni, imeanza vema mashindano ya Copa-Coca-Colakwa U-15,  ngazi ya taifa baada ya kuifunga Arusha mabao 3-1 kwenye mchezo uliochezwa katika uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam jana.
Arusha ndio walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 38 lililofungwa na mshambuliaji Robert Philipo lakini mshambuliaji wa Kinondoni Rashid Kilongola alisawazisha bao hilo katika dakika ya 48.
Baada ya mabao hayo timu zote zilishambuliana kwa zamu lakini bahati ilikuwa ya Kinondoni kwani walifanikiwa kupata bao la ushindi katika dakika ya 85 lililofungwa na Rashid Kilongola.
Akizungumza baada ya mchezo kocha wa timu ya Arusha, Mohamed Laiser alisifu kiwango cha wachezaji wake na kusema wamefungwa kwa bahati mbaya kwani walitawala mchezo kwa kipindi chote.
“Mchezo uliokuwa mzuri na wachezaji wamecheza vizuri lakini tuna nafasi ya kusonga mbele kwani timu yangu ni nzuri ila ni matokeo tu ya mpira hayo”, alisema Laizer
Michuano hiyo ilizinduliwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Fenella Mukangara juzi, ambaye aliwashauri makocha wa timu kutumia michuano ya Copa-Coca-Cola kama changamoto ya kuibua vipaji vipya katika timu zao kwa wasichana na wavulana.
Copa-Coca-Cola ni michuano pekee ambayo huanzia ngazi ya chini kabisa na baadaye ngazi ya Taifa ikishirikisha mikoa yote ya Tanzania bara pamoja na Zanzibar ambapo mwaka huu katika kuonesha umakini kwenye umri wamewaondoa wachezaji 87 kutoka katika mikoa ya Mbeya na Lindi kutokana na kudanganya umri.
Michuano hii itafikia tamati mnamo Desemba 20, mwaka huu, katika Uwanja wa kumbukumbu ya Karume jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment