Wayne Rooney akishangilia bao lake la mkwaju wa penati baada ya kusawazisha bao na kuweka 1-1 kwa bao walilokuwa wamejifunga wao wenyewe kupitia kwa Jordan Henderson usiku huu tarehe 15.11.2014 na Mtanange huo kumalizika kwa 3-1, England wameibuka Kidedea.
Wayne Rooney Usiku huu Uwanjani Wembley amecheza Mechi yake ya 100 wa England na pia kuwanasua toka Goli 1 nyuma na kusawazisha walipocheza na Slovenia Mechi ya Kundi E na hatimae kushinda Bao 3-1.
Kabla ya Mechi kuanza, Rooney alikabidhiwa Kofia ya Dhahabu na Sir Bobby Charlton ikiwa ni Tuzo kwa kuichezea England Mechi 100.
Danny Welbeck aliwaongezea bao la pili England na kufanya 2-1 katika kipindi cha pili hiho hicho katika dakika ya 65.
Danny Welbeck alifunga bao lake la pili tena na kufanya 3-1 katika dakika ya 72. Ushindi huu umeifanya England ipae kileleni ikiwa na Pointi 12 ikifuatiwa na Lithuania na Slovenia zenye Pointi 6 kila moja.
No comments:
Post a Comment