YAYA TOURE AWACHEFUA MASHABIKI KWA KUMKUMBATIA PEP GUARDIOLA
MASHABIKI
wa Manchester City wamemjia juu Mchezaji wao Yaya Toure kwa kitendo
chake cha kukumbatiana kwa furaha na Kocha wa Bayern Munich Pep
Guardiola Jumatano Usiku Uwanjani Allianz Arena mara tu baada ya City
kuchapwa Bao 1-0 kwenye Mechi ya Kundi lao la UEFA CHAMPIONS LIGI.Huku
Wachezaji wenzake wa City wakikumbwa na majonzi makubwa baada ya
kufungwa Bao la Dakika ya 89 la Shuti kali la Jerome Boateng, Toure
alitoka Uwanjani na kwenda moja kwa moja kucheka na kukumbatiana na
Guardiola ambae alikuwa Kocha wa Barcelona wakati Toure anachezea Timu
hiyo huko Spain. Kitendo
hicho kiliamsha hisia kali za Mashabiki wengi wa Man City ambao
walivamia Mitandao ya Kijamii na kumshutumu vikali Kiungo huyo ambae pia
amedaiwa kucheza chini ya kiwango kwenye Mechi hiyo. Hadi
sasa Man City imekataa kuzungumza chochote kuhusu sakata hili lakini
inategemewa Toure atacheza Mechi yao ijayo Uwanjani Etihad watakapoivaa
Chelsea kwenye Mechi ya Ligi Kuu England hapo Jumapili.Yaya Toure akiwa hoi baada ya kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Bayern Munich BAYERN vs CITY DISTANCE STATS Alonso 12.09km (7.51 miles) Alaba 11.44 (7.11) Gotze 11.41 (7.09) Lahm 11.29 (7.02) Silva 11.10 (7.02) Navas 11.07 (6.88) Toure 10.89 (6.77) Fernandinho 10.65 (6.62) Sagna 10.37 (6.44)
No comments:
Post a Comment