Pages

Saturday, September 20, 2014

TFF:YANGA LETENI RASIMU YA KATIBA


Pichani juu ni sehemu ya wanachama wa klabu Yanga waliopitisha katiba mwezi Juni.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeitaka klabu ya Yanga kuwasilisha rasimu ya Katiba waliyoipitisha, kwa kuzingatia kuwa Muhtasari wa kikao cha Mkutano Mkuu wao wa Juni 1 mwaka huu umeainisha baadhi ya marekebisho waliyofanya kwa tulivyowaelekeza.
Yanga wanatakiwa kuwasilisha rasimu hiyo kabla ya Oktoba 5 mwaka huu. Ikiwa itakubaliwa na TFF, itapelekwa kwa Msajili wa Klabu na Vyama vya Michezo ili waweze kufanya uchaguzi wa viongozi wao.

No comments:

Post a Comment