RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) Jamal Malinzi
anatarajiwa kufunga semina ya uongozi na utawala kwa viongozi wa soka la
wanawake Tanzania.
Semina hiyo ambayo ilianza Septemba 22 mwaka huu, inafanyika
kwenye ofisi za Karume, inashirikisha
viongozi 46 wa soka la wanawake kutoka
mikoa yote wanachama wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)
Akizungumza na gazeti hili msimamizi mwendeshaji wa semina
hiyo, Mkufunzi Henry Tandau alisema kuwa lengo la semina hiyo ni kuwaweza
viongozi wa soka la wanawake kuwa na uelewa wa jinsi ya kuendesha shughuli za
kila siku zinazohusu soka kwenye mikoa yao.
“TFF imetoa semina hii ili kutoa mwanga wa jinsi ya kuongoza
na kuendesha soka la wanawake kwenye mikoa yote ya Tanzania”, alisema Tandau.
Pia alisisitiza kuwa TFF imedhamiria soka la wanawake liende
sambamba na soka la wanume ndio maana wameamua kuwaita viongozi wa soka la
wanawake ili wakashirikiane na viongozi wa mikoa kuinua soka katika wilaya
baadae ipatikane timu bora ya wanawake yenye sura ya kitaifa.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi, Wilfred Kidau alisema
kuwa semina hii ni muhimu kwani itasaidia kuinua soka la wanawake ili liendane
na nchi Nigeria, Afrika ya Kusini, Ghana na nyingine ambazo zimefanikiwa kwenye
Nyanja ya soka la wanawake.
“Semina hii itasaidia kuinua soka letu liendane na wenzetu
Afrika ambao wemeendelea kwani ina lengo la kuwasaidia kuibua vipaji, kutafuta
wadhamini, kuandika pendekezo pia kujua kanuni zinazoendesha mashindano”,
alisema Kidau.
Semina hii pia inawasaidia kwenda kusimamia kuandaa timu
ambayo itashiriki ligi ya wanawake inayotarajiwa kuanza hivi karibuni, ligi
ambayo itashirikisha mikoa yote wanachama wa TFF.
No comments:
Post a Comment