WACHEZAJI WAPYA wa Manchester United,
Radamel Falcao na Daley Blind, Leo hii wametambulishwa rasmi mbele ya
Wanahabari huko Old Trafford Jijini Manchester United wakiwa pamoja na
Meneja wa Klabu yao Louis van Gaal.
Falcao
ndie aliejibu swali la kwanza na kusema: “”Nina furaha kubwa kuwa hapa.
Ni changamoto kubwa katika maisha yangu ya Soka. Siku zote nimekuwa na
ndoto ya kuwa kwenye Klabu kama Man United.” Akijibu swali aliloulizwa
kuhusiana na kuumia vibaya Goti lake mwanzoni mwa Mwaka huu, Falcao,
Mchezaji wa Kimataifa wa Colombia aliehamia kutoka AS Monaco kwa Mkopo
wa Msimu mmoja ambao unaweza kuwa wa kudumu, alisema: “Najisikia vyema.
Nilianza tena kucheza Miezi miwili iliyopita na Monaco na nimekuwa bora
zaidi Mwezi uliopita na kufunga Mabao kadhaa ambacho ni kitu muhimu kwa
Mastraika. Sina tatizo na Goti langu.”
Nae Blind, aliehamia kutoka Ajax na
ambae alikuwa mmoja wa Wachezaji wa Van Gaal kwenye Kikosi cha
Netherlands kwenye Kombe la Dunia, aliulizwa kuhusu uhusiano wake na Van
Gaal na akasema: “Ni Mtu mkali na wa moja kwa moja. Wachezaji ni lazima
wafuate kile kile ili kushinda gemu. Anasoma Mchezo vizuri na utabiri
wake ulikuwa sahihi karibu kila Gemu kwenye Kombe la Dunia!”
Radamel Falcao kwenye mazoezi
No comments:
Post a Comment