Mshambuliaji
wa zamani wa Yanga aliyehamia kwa mabingwa wa soka Tanzania Bara wana
lamba lamba Azam fc Didier Kavumbagu amewachana wachezaji wa timu yake
hiyo ya zamani kuwa wana tabia ya ubinafsi na kujifikiria wao wenyewe na
si timu, jambo ambalo lilimfanya ashindwe kufunga magoli mengi
alipokuwa na timu hiyo msimu uliopita.
Kavumbagu
ambaye aliifungia Azam magoli mawili kati ya matatu katika mchezo wa
ufunguzi wa pazia la ligi kuu msimu huu dhidi ya Polisi Tanzania
Jumamosi iliyopita, amesema tabia ya uchoyo ilikuwa ni tatizo kwake
kwasababu kila mtu alikuwa anataka kufunga goli hata kama hakuwa katika
nafasi ya kufunga.
Akiongea
na mtandao huu wa habari wa Rockersports, Kavumbagu bila ya kung'ata
maneno amesema hilo ni tatizo sugu ndani ya kikosi cha Yanga na kwamba
litaigharimu timu hiyo katika msimu huu endapo halitamalizwa.
Ingawaje
hakuwa tayari kuwataja wachezaji kwa majina yao, mshambuliajia huyo
raia wa Burundi alionekana kufunguka kwa kusema mchezaji anayefanya
hivyo anajijua endapo atasikia habari hizi.
Msimu
uliopita katika safu ya ushambuliaji ya Yanga mshambuliaji huyo alikuwa
akishirikiana na Simon Msuva, Gerson Tegete, Hamisi Kiiza, Mrisho
Ngasa, Saidi Bahanuzi, Hussein Javu,Haruna Niyonzima, Nizar Khalfani na
Emmanuel Okwi.
Amesema
anatarajia kufunga magoli mengi zaidi kuliko msimu uliopita alipokuwa
na Yanga kwa kuwa kikosi cha Azam fc kinawachezaji wazuri na
wanashirikiana wanapokuwa katika mwendo wa kuelekea katika goli la
mpinzani.
Amewataka
mashabiki wa Azam fc kuendelea kumpa sapoti kwakuwa amekwenda Azam
kufanya kazi na wategemee kuona kazi yake nzuri ndani ya kikosi hicho.
No comments:
Post a Comment