Pages

Wednesday, September 3, 2014

DAVID BECKHAM ASIKITIKA WELBECK KWENDA ARSENAL WAKATI TOM CLEVERLEY AHAMIA ASTON VILLA KWA MKOPO

UHAMISHO uliochelewa wa Kiungo wa Manchester United Tom Cleverley kwenda Aston Villa kwa Mkopo wa Msimu mmoja umebarikiwa hii Leo wakati Lejendari wa Man United David Beckham amesikitishwa kuondoka kwa David Welbeck kutoka Man United kwenda Arsenal.
Dirisha la Uhamisho lilifungwa rasmi Jana Usiku lakini Uhamisho wa Cleverley ulichelewa lakini hivi sasa Bodi ya Ligi Kuu imeubariki. 

Makubaliano kati ya Man United na Aston Villa yana vipengele kwamba Cleverley, mwenye Mkataba na Man United hadi 2015, anaweza kurudi Old Trafford Mwezi Januari au Villa imsaini kwa kudumu katika Kipindi hicho cha Usajili.
Cleverley, mwenye Miaka 25, amekulia toka Vyuo vya Soka vya Man United tangu akiwa mdogo na kuichezea Klabu hiyo Mechi 79.

David Beckham amesikitishwa na kuondoka kwa Danny Welbeck na kuhamia Arsenal.
Beckham amesema Arsenal wamepata dhahabu kwa kumnunua Welbeck na kuonyeshwa kusikitishwa kwake kumpoteza Mchezaji aliekuzwa kipaji toka Chuo cha Soka cha Man United tangu akiwa na Umri wa Miaka 8.

Beckham amesema: “Ni wazi kumwona Danny kuondoka, kwa mimi Shabiki wa Man United, kunasikitisha lakini mie si Meneja!”

No comments:

Post a Comment