Pages

Wednesday, August 6, 2014

Totternham katika mazungumzo na Villareal kwa ajili ya mlinzi Mateo Musacchio


Mateo Musacchio
Uongozi wa klabu ya Tottenham upo katika mazungumzo na klabu ya Villarreal kwa ajili ya kutaka kukamilisha mpango wa kumsajili beki kutoka nchini Argentina Mateo Musacchio.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewana kituo cha televisheni cha SKY SPORTS cha nchini UIngereza, Tottenham wameanzisha mazungumzo hayo huku wakiamini kiasi cha paund million 17 kitatosha kukamilisha usajili wa beki huyo mwenye umri wa miaka 23.

Sifa kubwa ambayo inatumiwa na Spurs kwa kutaka kumsajili Mateo Musacchio ni faida ya kucheza katika nafasi ya beki wa kati na pia kucheza katika nafasi ya beki wa pembeni hivyo wanaamini endapo watamsajili watakuwa wametimiza malengo ya kuziba nafasi mbili kwa mchezaji mmoja.

Mpaka sasa Mateo Musacchio tayari ameshaitumikia klabu yake ya Villareal katika michezo 32, ambapo inaaminiwa ni kipimo kizuri kwake katika harakati za kuhamishia uwezo wake kwenye ligi ya nchini Uingereza.

Meneja mpya wa klabu ya Tottenham Mauricio Pochettino, tayari ameshakamilisha usajili wa wachezaji wanne ambao anaamini watakiboresha kikosi hicho ambacho msimu uliopita kilikuwa chini ya meneja Tim Sherwoods.

Wachezaji waliosajiliwa na Spurs katika kipindi hiki ni Ben Davies, Michel Vorm pamoja na Eric Dier huku beki wa kati kutoka nchini Ubelgiji Jan Bert Lieve Vertonghen akihusishwa na taarifa za kutaka kuihama klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment