Pages

Saturday, August 2, 2014

NI MUDA WA KUTUMIA VIKUBWA ILI UPATE VIKUBWA

Baada ya Liverpool kuachana na mpango wa kumsajili mshambulizi Loic Remy nadhani plan B si kurejea tena Southampton kumsajili Jay Rodriguez.
Nasema siyo Rodriquez kwasababu kama ni usajili wa ligi kwa asilimia fulani Liverpool wameshaukamilisha lakini linapokuja suala la ligi ya mabingwa hapo ndipo ninapo ukataa usajili wa Jay Rodriguez na kuutaka usajili mkubwa zaidi ya huo.
Nimekitazama vizuri kikosi cha Brendan Rogers na kubaini idadi kubwa ya wachezaji wa safu ya mbele hawana uzoefu name
ligi ya mabingwa anzia Raheem njoo kwa Lambert kisha rudi kwa Coutinho na mwisho Sturridge na Markovic hawa wawili kidogo wanaujua ugumu wa huku.
Sina hofu na safu za kiungo wala ulinzi kwani wengi walishakipiga sana tu katika michuano hiyo mfano Glen Johnson,Habib Kolo Toure,Martin Skter pamoja na Daniel Agger.
Hofu yangu ni kuwa approach ya ligi kuu na ile ya mabingwa ni vitu viwili tofauti ndiyo maana msimu uliopita vilabu vya Chelsea,Arsenal,Man City na Man United vilitoka patupu licha ya kuwa tishio nyumbani (isipokuwa vijana wa zamani wa Moyes)
Brendan Rodgers anapaswa kuachana na ndoto za kumsajili Rodriguez ambaye mi namuona ni average player na badala yake alete world class players mfano Jackson Martinez,Klass Jan Huntelaar,Edinson Cavan na wengineo wengi ambao watakuja kuleta uimara na kupunguza hofu kwa vijana wageni kama Raheem na Coutinho.
Ligi ya mabingwa kuna mabeki vichaa kama akina Pepe,Chiellini,Bruno Alves hivyo kupata pointi tatu unahitaji a proven striker siyo anayekwenda kujifunza vingine mtatoka mapema kama ilivyofanya timu yenu ya Taifa kwenye Brazuka.
Habari hii imeandikwa na Paul Manjale kwenye mtandao wa Facebook

No comments:

Post a Comment