Pages

Saturday, August 23, 2014

LIVERPOOL YAMLEGEZA BALOTELLI KWA BONUSI KUBWA LAKINI YAMTEGA KWENYE MKATABA KINIDHAMU HUKU MASHABIKI WA LIVERPOOL WAKIPAGAWA


Balotelli alipanda Ferrari yake huko Brescia akijiandaa kwa safari ya kuelekea Liverpool
Liverpool imempa Mario Balotelli kivutio kikubwa cha fedha kwa matumaini kuwa itasaidia katika kukidhi mahitaji yake pamoja na kujituma zaidi ndani ya Anfield.
Baada ya liverpool kukubali kutoa ada ya pauni milioni £16 kwa AC Milan na kushikilia mpango wao wa kukutana na wakala wa mchezaji huyo Mino Raiola, tayari Balotelli ameshakwea pipa kuelekea Manchester tangu jana kwa ajili ya vipimo vya afya na kukutana na ana kwa ana na meneja wa Liverpool Brendan Rodgers kwa mara ya kwanza. 
Mamia ya mashabiki wa Liverpool walijitokeza kumlaki katika uwanja wa mazoezi wakati akiondoka ikiwa ni ishara kuwa ayapata mapokezi mazuri atakapo tua rasmi Anfield. endapo mambo yote yatakwenda vizuri mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Italia basi atasaini mkataba wa miaka mitatu utakao kuwa na thamani malipo ya kati ya pauni £85,000 mpaka £90,000 kwa wiki. 
Lakini pamoja na hayo anatarajiwa kupata bonasi ya ambayo itakuwa ndani ya mkataba ambayo kimsingi itapelekea kumfanya asichomoe kuingia mkataba na klabu hiyo.
Mario fever: Balotelli meets fans outside Melwood training ground after talks over £16m move from AC Milan


Balotelli amekutana na mashabiki nje ya uwanja wa mazoezi wa Liverpool wa Melwood baada ya mazungumzo ya uhamisho wake wenye thamani ya pauni milioni £16 akitokea AC Milan


On the way: Balotelli leaves Melwood training ground after talks on Friday
Akiwa njiani: Balotelli akiondoka uwanja wa mazoezi wa Melwood baada ya mazungumzo ya hao jana Ijumaa
Friday fun: Hundreds of fans gathered outside training ground to catch a glimpse of Balotelli
Mamia ya mashabiki wa Liverpool wakiwa wamekusanyika nje ya uwanja wa mazoezi kwa lengo la kujionea wenyewe mshambuliaji wao mpya Balotelli
Super striker: Balotelli arrives at Melwood for talks after flying from Italy in private jet
Super striker: Balotelli akiwasili Melwood kwa mazungumzo baada ya kusafiri akitokea Italia kwa ndege binafsi

Inaarifiwa kuwa mkataba huo pia umeingizwa vifungu ambayo vitahusisha hatua za kidhamu ambazo zinaweza kuchukuliwa kwa mchezaji huyo endapo atakwenda kinyume.
Swali ni je Balotelli atajiepusha na matatizo? Lakini pia kipo kifungu ambacho kinaipa uwezo Liverpool kuchagua kumuongezea mwaka mmoja ndani ya mkataba wake huo.

Rodgers amekataa kuulizwa maswali kuhusu Balotelli katika mkutano wake na waandishi wa habari lakini amesisitiza kuwa mazingira magumu aliyoyajenga kwa miaka miwili iliyopita ni imara kiasi kumuingiza kila mtu mpya ndani yake na kufanana nayo.

No comments:

Post a Comment